Nigeria yapiga kura,Je hali ikoje?

Image caption Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na mpinzani wake Muhammadu Buhari

Raia wa Nigeria wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa urais na ubunge ,licha ya visa vichache vya ghasia na matatizo ya kiufundi.

Takriban watu 20 wameuawa katika mashambulizi ya jimbo la Gombe yanayoshukiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram.

Image caption Wapiga kura Nigeria

Tume ya uchaguzi imesimamisha shughuli za kupiga kura katika baadhi ya maeneo kufuatia matatizo ya kiufundi yaliokumba kifaa cha kutambua kadi za wapiga kura.

Tume hiyo imesema kuwa shughuli hiyo itaendelea siku ya jumapili.

Image caption nigeria

Rais Goodluck Jonathan ambaye anaomba kuchaguliwa kwa awamu ya pili anakabiiwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari.