Matatizo ya kiufundi yaathiri uchaguzi

Image caption Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan akiongoea na wanahabari baada ya kushindwa kujisajili kutokana na sababu za kiufundi zinazokabili vifaa vya uchaguzi

Raia wengi wa Nigeria wamechelewa kupiga kura ya kumchagua rais wa taifa hilo.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa matatizo yameibuka kwenye vifaa vya mkononi ambavyo hutumiwa kusoma kadi za kupigia kura.

Rais Goodlack Jonathan ni miongoni mwa watu walioathiriwa na tatizo hilo swala lililomfanya usubiri nje ya kituo cha kupigia kura kwa mda.

Pia kuna ripoti za kutimuliwa kwa waangalizi kutoka kwa vituo vya kupigia kura na maafisa wa chama tawala.

Rais Jonathan anakabiliwa na upinzani mkali kutoka aliyekuwa kiongozi wa utawala wa kijeshi Muhammadu Buhari.