Makabiliano Hotelini Somalia yamalizika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makabiliano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Al Shabaab katika hoteli ya Al Mukarama yamemalizwa kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Somalia

Maafisa wa serikali ya Somalia wanasema kuwa mapigano yalikuwa kwenye hoteli moja mjini Mogadishu kufuatia uvamizi wa wanamgambo wa Al shabaab yamemalizika.

Maafisa hao walisema kuwa wanajeshi wa serikali waliingia eneo hilo kuidhibiti hoteli ya Maka al Mukarama zaid ya saa 12 baada ya wanamgambo kuivamia.

Watu 9 waliuwa wakati wa uvamizi huo akiwemo mjumbe mmoja wa Somalia.

Waandishi wa habari eneo hilo wanasema kuwa miili ya wanamgambo na ya wanajeshi ilikuwa eneo hilo.

Wataalamu wa kutegua mabomu wanasaka hoteli hiyo kujua iwapo kuna milipuko yoyote.