James Bond akana kum'bagua Idris Elba

Haki miliki ya picha PA
Image caption Aliyekuwa James Bond Roger More

Aliyekuwa nyota wa filamu ya 007 Roger More ama kwa jina la usanii James Bond amesema kuwa madai kwamba alitoa tamko la kiubaguzi dhidi ya msanii Idris Elba si ya kweli.

Akizungumza na jarida moja la Ufaransa Paris Match.

Bond anasema kuwa aliulizwa kuhusu Elba kumrithi Daniel Craig ambaye ndiye anayeigiza kama James Bond.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Idris Elba

Msanii huyo wa filamu wa mda mrefu,alinukuliwa akisema kuwa mtu anayefaa kumrithi katika filamu mpya ya 007 anafaa kuwa ''English-English''.

Matamshi hayo yalizua hisia kali kutoka kwa watu wa mitandaoni lakini akasisitiza kuwa alinukuliwa vibaya.

''Ijapokuwa nafasi ya James imechezwa na raia wa uskochi,wa Wales na Ireland nadhani ni vyema akisalia kuwa Muingereza'',alisema Bwana Roger Moore.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Idris Elba

Mnamo mwezi Disemba mwaka 2014, kufuatia uvamizi wa mtandao wa SONY ,lilidaiwa kuwa mwenyekiti wa Amy Pascal alimpendekeza Idris Elba kumrithi Roger Mora kama james Bond.