Mazishi ya Lee Kuan Yew yafanyika

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeneza la mwanzilishi wa taifa ya Singapore marehemu Lee Kuan Yew

Mazishi ya mwanzilishi wa taifa la Singapore Lee Kuan Yew yanafanyika.

Jeneza lake lilisafirishwa kwenda chuo kikuu kupitia barabara za mji ambapo maelfu ya watu walivumilia mvua kubwa kutoa heshima zao za mwisho.

Lee Kuan Yew anazikwa kwa heshima zote ikiwemo mizinga 21 na kimya cha dakika moja.

Mazishi yake yanahudhuriwa na viongozi wa eneo hilo pamoja na aliyekuwa rais wa marekani Bill Clinton

Lee Kuan Yew aliongoza Singapore kwa zaidi ya miaka 30.

Amelaumiwa kwa kuiongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma lakini pia amesifiwa kwa mafanikio yake ya kiuchumi.