Upigaji kura waendelea Nigeria

Image caption maeneo mengi yanahesabu kura zilizopigwa

Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Nigeria unaendelea kwenye vituo kadha kwa siku ya pili kutokana na kuwepo matatizo ya kiufundi kwa vifaa vya kukagua kadi za kura jana jumamosi.

Katika sehemu nyingine mamilioni ya wapiga kura walipiga kura kuchagua kati ya rais Goodluck Jonathan na kiongozi wa zamani wa kijeshi Mohammadu Buhari.

Uchaguzi huo ulikuwa umeahirishwa kwa wiki sita kutokana na harakati za kundi la Boko Haram.

Mashambulizi kadha katika eneo la kaskazini mashariki la Gombe yalivuruga upigaji kura na kusababisha vifo vya karibu watu 20.