Upigaji kura waendelea Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shughuli ya kupiga kura yaendelea katika maeneo kadhaa nchini Nigeria

Katika uchaguzi mkuu wa Nigeria, watu wanaendelea kupiga kura kwa siku ya pili katika baadhi ya vituo, kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyotokea jana.

Vifaa vya kusoma vitambulisho, vilivyokusudiwa kuzuia udanga-nyifu, viliharibika, na kuchelewesha upigaji kura.

Lakini katika maeneo mengine, mamilioni ya wa Nigeria walipiga kura bila ya tatizo.

Mashindano ni makali baina ya wagombea wawili wakuu wa urais, Goodluck Jonathan na kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari.

Wanajeshi wa Nigeria hivi sasa wanapambana na wapiganaji kadha wa Boko Haram, nje ya mji wa Bauchi, kaskazini-mashariki mwa nchi.