Wanigeria wasifiwa kwa uvumilivu

Mama Patience Jonathan akipiga kura Jumamosi Haki miliki ya picha bbc

Wanigeria wamepata sifa nyingi kwa namna walivyopiga kura katika uchaguzi Jumamosi ingawa kulikuwa na matatizo ya kiufundi.

Zana za elektroniki za kusoma kadi za vitambulisho ziliharibika na kuchelewesha upigaji kura.

Mkuu wa ujumbe wa wasimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuia ya Afrika Magharibi, ECOWAS, John Kufuor, aliwasifu Wanigeria kwa ustahmilivu wao.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, aliwapa hongera kwa kuendesha upigaji kura kwa salama na mpango, na aliwaambia wameonesha uvumulivu huku wanakabiliwa na ghasia za wapiganaji Waislamu.

Upigaji kura unaendelea kwa siku ya pili katika vituo vilivyoathirika na matatizo ya kiufundi.