11 wauawa Brazil katika uporaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa Brazil

Idara ya usalama nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa wakifanya jaribio la kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Taarifa hizo zinasema kuwa majambazi hao walianza kurushiana risasi na Polisi katika mji wa Novos Kaskazin Mashariki mwa Brazil. Mtu mmoja anashikiliwa na Polisi,ambapo pia bunduki na vifaa vya milipuko vilivyokuwa vinamilikiwa na watu hao vinashikiliwa. Katika tukio jingine pia Polisi wamewaua watu wengine wanne wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika mji wa Rio de Janeiro. Kuuawa kwa majambazi hao kunafuatia mapambano ya polisi na kundi hilo,ambapo mabomu na Bunduki vilikamatwa pia.