Obama kuzuru Kenya Julai

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama kuzuru Kenya Julai

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Barrack Obama atazuru Kenya mwezi Julai mwaka huu, taifa alikozaliwa babake.

Inasemekana kuwa Bwana Obama, atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu ujasirimali, utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo-Nairobi.

Tangu awe Rais wa Marekani, Barack Obama hajawahi kuzuru taifa hilo la Afrika Mashariki kama Rais.

Image caption Obama, atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu ujasirimali

Alizuru mataifa kadhaa za Afrika ikiwemo ziara ya taifa jirani Tanzania mnamo mwaka 2013 bila kuzuru Kenya.

Alizuru Kenya akiwa seneta mnamo mwaka 2006.

Bababke Obama alisomea Marekani na hatimaye kurejea Kenya baada ya Obama kuzaliwa.