Mjukuu wa hayati mzee Mandela ahukumiwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mandla Mandela apatikana na hatia huko Afrika Kusini

Na mahakama Nchini Afrika Kusini yamemhukumu mwanawe wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Nelson Mandela, Mandla Mandela, kwa kumjeruhi mtu.

Mandla Mandela, ambaye ni mbunge, alihusika katika kisa cha barabarani mnamo mwaka 2013 na kisha akachomoa bastola.

Mapema mwaka huo huo huo, mzozo kuhusu mahala pa maziko kwa familia ya Mandela, pia iligonga tena vichwa vya Habari.