Msimamo kuhusu Iran watofautiana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wajumbe wa mazungumzo ya Nyuklia

Wajumbe wa mazungumzo ya mpango nyuklia wa Iran wanaokutana nchini Switzerland wametofautiana misimamo yake katika mkutano ulioendelea hadi usiku wa leo.

Wakati Waziri Mkuu wa Urusi Sergei Lavrov, akisema mazungumzo hayo yamefikia maamuzi katika mambo yote ya msingi kuhusiana na suala la Iran,Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif yeyeanasema alitaraji kuwa wangeanza kuanda rasmu ya mapendekezo. Lakini ujumbe kutoka nchini Marekani unasema kuwa si mambo yote ya msingi kuhusiana na mpango wa Iran yameorodheshwa katika mkutano,wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akidai kuwa analazimika kuondoka mkutanoni hapo kuwahi mkutano mwingine mjini Paris.