Buhari aapa kulitokomeza Boko Haram

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Goodluck Jonathan na Muhammadu Buhari

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameelezea mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kama tatizo kuu linalokabili taifa hilo.

Katika hotuba aliyotoa katika runinga za Nigeria,kiongozi huyo wa kijeshi zamani amesema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi kuangamiza ugaidi.

Vilevile amesema kuwa atakabiliana na jinamizi la ufisadi.

Bwana Buhari ambaye anachukua wadhfa wa urais kuanzia mwezi ujao,alimsifu mpinzani wake na rais anayeondoka Goodluck Jonathan.

Alimtaja kuwa kiongozi anayehitaji heshima.