Ubakaji kukomeshwa,DR Congo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa DR Congo

Makamanda wa jeshi la Jamhuri ya Demokasi ya Congo,wamesaini maazimio yanayolenga kukomesha vitendo vya ubakaji katika maeneo ya vita.

Kutokana na maazimio hayo kila kamanda wa Jeshi atapaswa kuheshimu makubaliano hayo kwa mjibu wa sheria za kupinga ubakaji na kuhakikisha wanajeshi katika vikosi vyao hawafanya vitendo hivyo

Maazimio hayo yamesainiwa mbele ya Mawaziri wa serikali na mwakilishi wa umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya unyanyaji wa kijinsia na migogoro, Zainab Hawa Bangura.

Bi.Zainab amesema kuwa hatua hiyo ni mwanzo katika kutokomeza ukatili kwa wanawake katika demokrasia ya Congo.