IS yadhibiti kambi ya wakimbizi Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Islamic state

Wapiganaji wa kundi la Islamic State nchini Syria wameingia na kuchukua udhibiti wa kambi kubwa ya wakimbizi wa Palestina ya Yarmouk kandokando ya mji mkuu wa Damascus.

Kambi hiyo ambayo ni nyumbani kwa watu elfu kumi na nane imekuwa ikipatikana katika mashambulizi ya udhibiti wa makaazi ya Damscus kati ya majeshi ya serikali na makundi ya waasi ambayo pia yanaipinga IS.

Kuna ripoti kutoka ndani ya kambi hiyo kwamba mapigano yanaendelea kati ya wapiganaji wa IS na makundi hasimu.

Maafisa wa umoja wa mataifa wameonya mwezi uliopita kwamba wakaazi wa kambi hiyo wanakabiliwa na hali ngumu huku wakikosa umeme,chakula cha kutosha pamoja na dawa.