Jimbo la California kukabiliana na ukame

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ukame ulilolikumba jimbo la California nchini Marekani

Serikali ya jimbo la California nchini Marekani limetoa amri ya kudhibiti matumizi ya maji katika jimbo hilo kwa mara ya kwanza katika historia yake ya kupambana na ukame.

Gavana wa jimbo la California, Jerry Brown analenga kupunguza matumizi ya maji kwa asilimia ishirini na tano.

Mamilioni ya mita za mraba za viwanja vya nyasi zinazotunzwa vizuri katika ardhi inayomilikiwa na serikali zitabadilishwa na kuwekewa majani yanayohimili ukame.

Gavana Brown ameyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari katika milima ya Sierra Nevada ambayo haina nyasi ambayo kwa kawaida wakati huu wa mwaka ingekuwa imefunikwa kwa theluji yenye kuzidi mita moja kwenda juu.