Murray atinga nusu fainali Miami Open

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray atinga nusu fainali Miami Open

Mcheza tenis wa Uingereza Andy Murray amefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kumshinda Dominic Thiem raia wa Austria katika mashindano ya Miami Open yanayoendelea huko nchini Marekani.

Pamoja na kupoteza seti ya kwanza ya mchezo huo,Murray alifanikiwa kuzinduka na kushinda kwa jumla ya seti 3-6 6-4 na 6-1.

Murray mwenye umri wa miaka 27, anaweza kupambana na Tomas Berdych raia wa Czech ama Muajentina Juan Monaco katika nusu fainali ya mashindano hayo.

Naye Serena Williams amepata ushindi wa 700 tangu aanze kucheza mchezo huo baada ya kuingia nusu fainali kwa kumbwaga mjerumani Sabine Lisicki.