Vigogo wa Siasa na mdahalo,Uingereza

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mdahalo wa viongozi Uingereza

Viongozi wa vyama vitano vya siasa nchini Uingereza wameshiriki katika mdahalo ulioonyeshwa moja kwa moja katika televishen ambao ulilenga maeneo mhimu katika harakati za kuijenga Uingereza.

Kila kiongozi katika mdahalo huo viongozi hao walipewa muda wa kujibu maswali kuhusu masuala ya kiuchumi,uhamiaji,afya na mtazamo ujao kuhusu Uingereza. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amekitetea chama chake cha Conservative kwamba kimekuwa na mipango mizuri ya kiuchumi na kukubali mapendeekezo yaliyotolewa na chama cha upinzani cha Labour.

Mwandishi wa BBC kuwa katyika mdahalo huo hakukuwa na mshindi,kwani hayo siyo yalikuwa malengo ya mkusanyiko huo,bali fursa ya kubainisha mamabo ya mhimu na kwamba hata baadhi ya vyama vidogo vingeweza kushiriki.