Nyuklia:Iran yaapa kutekeleza makubaliano

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hassan Rouhani

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema nchi yake itatekeleza wajibu wake kikamilifu kuhusiana na muafaka uliofikiwa kuhusiana na mpango wake wa kupata nguvu za nyuklia mradi tu wahusika wengine kwenye makubaliano hayo watekeleze wanayopasa kuyafanya.

Akihutubia taifa hilo kupitia runinga ya nchi hiyo, rais Rouhani ameongeza kusema mataifa 6 makuu duniani yaliyoshiriki katika majadiliano hayo walikubali kuwa Iran ina haki ya kuendelea na mpango huo ndani ya mipaka yake na bila kuhatarisha usalama wa mataifa mengine.

Chini ya makubaliano hayo Iran imekubali kupunguza kiwango cha mradi huo kwa zaidi ya theluthi mbili.