Amri ya kutotoka nje yatolewa Garissa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Serikali imetoa amri ya kutotoka nje Garissa Kenya

Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotoka nje usiku kwa muda wa wiki mbili katika kaunti kadhaa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Amri hiyo iliyotolewa na mkuu wa polisi nchini humo, imetolewa baada ya wanamgambo wa kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia kuwaua zaidi ya watu 147.

Mbunge wa eneo hilo, ambaye pia ni kinara mkuu wa upande wa wanasiasa wengi bungeni, Aden Bare Duale, ameiambia BBC kuwa Waziri wa maswala ya ndani ya taifa anafanya mkutano wa dharura wa usalama mjini Garissa.

Serikali imetoa zawadi nono kwa mtu atakayetoa ripoti ya kukamatwa kwa mhusika mkuu katika shambulio hilo.