Wajivunia kuwa makahaba Australia

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wafanya biashara ya ngono wakiwa kazini

Hivi umeshawahi kujiuliza kwamba wafanyabiashara ya ngono ni watu wa namna gani? Ama biashara hiyo ni biashara kama biashara zingine kivipi? Nchini Australia,maelfu ya wafanyabiashara ya ngono bila soni wameweka bayana namna wanavyotumia mitandao ya kijamii na kuueleza ulimwengu jinsi wanavyo fanikisha biashara hiyo.

Huwa hawachagui wateja,Mwanafunzi mwenzangu? Mwanasheria nimtakaye,mwanaharakati,binti yangu?dada yangu, mfanya biashara mwenzangu wa ngono? Familia yangu! Sihitaji msaada wao.

Huo ni baadhi ya maelfu ya ujumbe kutoka nchini Australia kwa wafanya biashara ya ngono wanaojieleza huku wakitumia ukurasa wa #facesofprostitution hashtag.Fukuto hili lilianza tangu mwishoni mwa juma lililopita katika Instagram na mfanya biashara wa ngono mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mhitimu wa masuala ya Historia anayejulikana kama Tilly Lawless.

Aliamua kuzungumzia blog moja iliyoamua kurudia kuweka kwenye ukurasa wake taarifa iliyorushwa wiki iliyopita katika ukurasa wa gazeti maarufu lenye kuandika habari za akina mama liitwalo, Mamamia.Blog hiyo iliandika katika maadhimisho ya miaka ishirini na mitano mkutano wa wafanya biashara ya ngono na filamu yao ya ‘prince-charming Pretty Woman' na kudai kuwa shuhguli nzima ya biashara ya ngono haina mvuto kama ilivyo katika filamu hiyo.

Tilly Lawless alichukizwa na namna taarifa hiyo ilivyoweka mambo kirahisi rahisi na kuijumuisha biashara ya ngono na kuiona biashara hiyo kama yenye madhara .bibi huyo anashuhudia kuwa ameifanya biashara hiyo ya ngono kwa miaka miwili lakini amejulikana hadharani miezi miwili iliyopita mjini Sydney,mahali ambako biashara ya ngono ruksa kuifanya kisheria . na alichukua maamuzi ya kuweka picha yake bayana katika ukurasa wake wa Instagram kuonesha uzuri na upande wa pili wa biashara ya ngono ,sura ya mwanamke mrembo,ambaye anajitambua na aliyechagua kuwa mfanyabiashara ya ngono kwa mantiki ya kukipinga kilichoandikwa katika jarida la Mamamia na blog pia.