Wakwe wanyweshwa mkojo kwa mwaka mmoja,

Image caption Machoni anatazamika, lakini moyoni alikuwa hana raha.

Mwanamke mmoja nchini India amekuwa na mazoe na tabia kujengeka ya kukojolea vikombe vya wakweze kila iitwapo leo kwa muda wa mwaka mmoja ,zake zilitimia baada ya kufumwa na mama mkwe wake jikoni akiwa amekinga buli la chai anakojoa ndaniye.

Chanzo kisa na sababu ya kadhia hiyo kutokea ni wakweze kumpiga marufuku mtoto wao wa kiume kufanya kazi za nyumbani na ndipo mkwe huyo alipoamua kujilipiza kisasi kwa kukojolea vikombe vya wakweze kwa zaidi ya mwaka mmoja.Rekha Nagvanshi, mwenye umri wa miaka 30,alikuwa akiishi nyumba moja yeye na mumewe Deepak,mwenye miaka 34, katika wilaya ya Indore jimbo la Madhya Pradesh,pamoja na wakweze .

Mwanamke huyo alidai kwamba ingekuwa bora angeishi na nduguze kuliko kuishi kwa wakeze,na alisema kwamba hakuwa na furaha namna ndoa yake ilivyoendeshwa na alikuwa akijihisi anatendewa visivyo na hapati matunzo muafaka.Rafiki wa mwanamke huyo , Alia Kohli, mwenye umri wa miaka 32, alisema kwamba rafikiye hakuwa na furaha na ndoa yake tangu siku ya kwanza ya harusi na mumewe alikuwa akimtenda kama mtumwa na mwanamke huyo ameamua kuwa imetosha.

Lakini chakushangaza baada ya kuondoka kuelekea kwa wazazi wake , mara aliomba kurejea ukweni ati tu kwasababu ya majaaliwa ya mtoto wao wa kike aliye na umri wa miaka minne ili aendelee kumpa malezi yake,na alipo rejea kwa wakweze aliweka masharti ya mumewe kumpikia chakula,kumkandakanda miguu yake na kumfulia nguo zake zote lakini wazazi wa kijana huyo hawakuridhishwa na masharti hayo ,hivyo waliweka mpango wa kukomesha masharti hayo.

Image caption Tabasamu usoni rohoni anakereketwa

Mume wa mwanamke huyo Deepak anasema kwamba yeye alikuwa radhi na masharti ya mkewe lakini wazazi wake walimjia juu na kumsema kwamba hiyo haikubaliki kwani anamshurtisha mtoto wao kama mtumwa.

hata hivyo inaelezwa kwamba,wazazi wa mwanaume huyo walikuwa na kawaida ya kuwatembelea watoto wao mara moja kwa wiki, kitendo kilichokuwa kikimkera mno mkamwana wao na akaamua kuwatenda, wazazi walipogundua hila yake walisema kwamba walijua mkwe wao hawapendi lakini hawakufikiria kwamba anaweza kuwatenda namna hiyo,maana alikuwa akitabasamu na kuwapa chai nao waliipokea,lakini siku moja mamake Deepak niliingia ghafla jikoni na kumfuma mkwe akikojolea birika ya chai.

wazazi hao mke Suraj na mume waliamua kwenda kutoa taarifa polisi ,na huko wakatwambia masuala ya namna hiyo hawashughuliki nayo,wazazi wa mwanaume huyo wakadai sheria ichukue mkondo wake maana si jambo rahisi kwa mwaka mmoja mtu akojolee birika yenye chai na aachiliwe hivi hivi, wanataka haki itendeke.

Kufuatia kisanga hicho imejulikana familia iko mbioni kulipeleka mahakamani suala hilo na kwamba Rekha na mumewe Deepak wametengana.