Yemen:Jumba la rais laachiliwa na waasi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumba la rais wa Yemen

Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa waasi wa Houthi wameondoka nyumba ya rais waliokuwa wameiteka katika mji muhimu wa kusini wa bandari ya Aden baada ya mshambulizi ya ndege za taifa la saudia kulenga eneo hilo.

Wapiganaji walio watiifu kwa rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wanasema kuwa wamepokea zana za kijeshi zilizoangushwa kutoka ndege za kijeshi za saudia wakati ambapo mapigano yanaendelea katika mji huo.

China imewaondoa zaidi ya raia wa kigeni 200 kutoka bandari hiyo.

Makumi ya raia yameripotiwa kuuawa siku chache zilizopita katika mapigano ya Aden.