Je,sheria za ndege Ujerumani zina dosari?

Image caption Maafisa wa ufaransa wakitafuta mabaki ya ndege ya Germanywings

Madai yameibuka kuwa shirika la usalama wa safari za ndege barani Ulaya lilielezea wasi wasi wake kuhusu kasoro kwenye sheria za usafiri wa ndege nchini Ujerumani kabla ya kutokea kwa ajali ya ndege ya shirika la Germanwings mwezi uliopita.

Shirika hilo liliiambia halmashauri ya safari za ndege ya Ujerumani mwezi Novemba kutatua matatizo yakiwemo ya uhaba wa wafanyikazi hali iliyotatiza shughuli za ukaguzi wa ndege pamoja na wafanyikazi wake.

Rubani Andreas Lubitz aliiangusha ndege yake makusudi ambapo abiria wote 150 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.

Utawala nchini ufaransa unasema kuwa umemaliza shughuli za kutafuta mabaki katika eneo la ajali.