Zimbabwe yatakiwa kutouza ndovu wachanga

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zimbabwe yashtumiwa kwa kuuza ndovu wachanga Uchina na Dubai

Serikali ya Zimbabwe inakabiliwa na shinikizo kali za kuitaka isitishe uuzaji wa ndovu wachanga kwenda nchini China na Dubai.

Makundi ya kulinda mbuga za wanyamapori yamelaani vikali biashara hiyo ya ndovu.

Serikali ya Zimbabwe inasema kuwa inawauza ndovu hao kwa sababu inaweza tu kuwakidhi ndovu 100,000 ambao kwa sasa wako kwenye mbuga zake.

Lakini mwenyekiti wa shirika la uhifadhi wa wanyama pori John Rodriguez ameiambia BBC kwamba idadi ya wanyama hao iko chini na kwamba ni ukatili kuwatenganisha ndovu wachanga na mama yao.