Mamia wauawa katika mgogoro wa Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wakiwa wameathirika kutokana na mgogoro nchini Yemen

Shirika la Afya Duniani limetoa takwimu zinazosaidia kuelewa ukubwa wa mgogoro uliopo nchini Yemen.

Shirika la WHO limesema karibu watu mia tano na hamsini wameuawa katika mapigano ya wiki za hivi karibuni, na kwamba watu wapatao elfu moja na mia saba wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Waasi wajulikano kama "houthi" na washirika wao wanapambana na majeshi ya Rais Abd Rabbu Mansour Hadi ambaye anaungwa mkono na jeshi la pamoja linaloongozwa na Saudi Arabia.

Baadhi ya mapigano makali yamekuwa katika bandari ya Aden, ambako mapigano ya mitaani yanaendelea huku yakiwa na athari zaidi kwa raia.