Jeremy Clarkson kurejea BBC

Image caption Jeremy Clarckson akiwa na tabasamu tele.

Wakuu wa sirika la utangazaji BBC wametangaza kuwa kipindi kijacho ambacho ni cha nne cha 'Have I Got News For You', kitatangazwa na Jeremy Clarkson.

Jeremy alikuwa mtangazaji wa zamani wa kipindi maarufu cha runinga pia cha 'Top Gear' atarekodi kipindi hicho kwa awamu tofauti tofauti na kitapeperushwa baadaye na kituo cha BBC2 mnamo April 24.

Msemaji wa mtangazaji huyo amesema kwamba mkataba wa Jeremy umesainiwa upya na Top Gear na mtangazaji huyo hajapigwa marufuku kuonekana katika runinga ya BBC.”

Jimmy Mulville, nguli wa runinga ambaye ni mmiliki wa Hat Trick, kampuni ambayo inazalisha kipindi hicho cha 'Have I Got News For You', amesema kwamba kipindi hicho kingepaswa kupeperushwa mwezi jana katikati ya vipindi vya Top Gear.

Lakini pia Jimmy hakusita kufanya mzaha kwamba pengine wanaweza kumpata mzalishaji ambaye hatathubutu kumtwanga ngumi Jeremy Clarkson akiwa runingani .

Shirika la utangazaji la BBC lilikataa kusaini mkataba mpya na Clarkson baada ya kugundua kuwa alimshambulia mmoja wa wazalishaji aitwaye , Oisin Tymon,wakati walipokuwa wakirekodi kipindi hicho cha runinga huko Yorkshire.

Mkurugenzi mkuu wa BBC Lord Hall,amesema kwamba mstari ushafungwa na hakuna kanuni moja kwa wote na kanuni moja kwa ajili ya mwingine.

Image caption Jeremy na wenzake katika moja ya vipindi vya Top Gear.

Na kauli ya mkurugenzi huyo pengine inafuatia polisi wa Yorkshire kuarifu kwamba kesi hiyo haina mashiko na haitasonga popote,na Clarkson hatakabiliwa na mashtaka yoyote kutokana na kitendo alichokifanya.

Na mzalishaji aliyeshambuliwa Tymon hakusita kutoa ya moyoni kwamba hakuwa na mpango wowote wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Clarkson.

Kurejea kwa Clarkson kwenye shirika la utangazaji la BBC kumethibitishwa na mipango ya James May na Richard Hammond wanaoendesha vipindi vya Top Gear ambao walisema kwamba vipindi hivyo vitaendelea kuoneshwa tena baadaye mwaka huu.