Mkenya ''atimuliwa kwa sababu ya rangi''

Image caption Mkenya ''atimuliwa kwa sababu ya rangi''

Mchezaji gofu ya kulipwa nchini Kenya‬ ametimuliwa mashindanoni baada ya kufoka kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa alikuwa amebaguliwa kwa msingi ya rangi yake katika klabu ya gofu ya Karen.

Hatua hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wapenzi wa gofu baada ya kudai kuwa alibaguliwa kwa misingi ya rangi yake katika klabu ya gofu ya Karen.

Kupitia mtandao wake wa Facebook Richard Ainley aliwaambia wafuasi wake kuwa alikuwa amebaguliwa alipokuwa akitaka kuegesha gari lake

kabla ya kushiriki mkondo wa kwanza wa mchuano wa Gofu ya kimataifa ya Kenya Open ulioanza mapema leo.

Mashindano hayo yanayoandaliwa kila mwaka ni sehemu ya ligi ya kimataifa ya gofu ya European tour.

Ainley alisema ''Looooo kumbe ukoloni bado upo Kenya !''

''Nimelazimika kutembea mwendo mrefu nikikokota gari langu la vigongo baad ya kunyimwa ruhusa ya kuegesha gari langu

ndani ya klabu ya gofu ya Karen licha ya kuwa mimi ni mkenya naambiwa kuwa ni Wazungu na waafrika wachahe tu wanaoruhusiwa kuingia humu''

hawajui kuwa mimi ni mchezaji wala hawataki kujua.

''Shindwe !Kwa hakika imenikera sana '' alifoka Ainley

Muda mchache baadaye Ainley aliitwa katika afisi za mwendesha mashindano wa klabu hiyo na kuelezwa kuwa alikuwa amekiuka sheria maadili na ustaraabu

wa klabu hiyo ya Karen na hivyo hatoruhusiwa kuendelea na mashindano.

''Nimekatazwa kuchezwa kwa sababu ukweli wa hali kama nilivyo andika awali katika mtandao wangu wa Facebook.

Nawaomba radhi wote niliowakwaza na kwa wale.

Kwa wachezaji wawakilishi wa Kenya waliosalia katika kinyang'anyiro cha Kenya Open mwaka huu nawatakia kila la kheri.

Hata hivyo afisa wa uhusiano wa mashindano hayo ya Kenya open bi Peggy Mwai ameiambia BBC kuwa si kweli kuwa Ainley alibaguliwa kwa misingi ya rangi bali ndiye aliyekiuka masharti ya mwaliko wake.

''Ainley alifika langoni akiwa amechelewa na hivyo aliwataka wale walinzi wa lango kuu la kuingia ndani ya Klabu ya Karen kumruhusu kuingia ndani na gari lake huku akifahamu fika kuwa hakuwa na cheti maalum chenye kumruhusu kuegesha gari lake ndani ya klabu''

''Walipokataa alifoka sana na kuwarushia keke na matusi ''aliongezea bi Peggy.

''Tumezungumza naye na tukamwonesha hali halisi kuwa alikuwa amekiuka sheria na masharti ya wageni waalikwa katika klabu mwenyeji ya Karen''

Na hapo mwaliko wake ukafutiliwa mbali.''

''Si Kweli kuwa alibaguliwa''

Mashindano hayo yalianza leo na yatakamilika siku ya jumapili.