Jaji na wakili wapigwa risasi Italy

Haki miliki ya picha AFP
Image caption shambulizi Milan

Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.

Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shambulizi la Milan

Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake.

Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi mjini Milan baada ya shambulio la mahakamani

Mshukiwa huyo alikamatwa kaskazini mwa Milan akitoroka kwa pikipiki.

Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.