Palestina waungana na Syria kuwatimua IS

Haki miliki ya picha EAP
Image caption Wakimbizi wa Palestina

Raia wa Palestina wanasema kuwa wamekubali kushirikiana na serikali ya Syria ili kujaribu kuwafurusha wapiganaji wa IS nje ya kambi moja ya wakimbizi viungani mwa Damascus.

Tangazo hilo hilo lilifanywa na afisa mmoja wa serikali ya Palestina huko West Bank.

Wapiganaji wa IS walitekeleza shambulizi katika kambi hiyo wiki iliopita na kuweza kuiyumbisha kanbi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa jeshi la Palestina.

Takriban wakimbizi elfu kumi na nane wanaishi katika kambi hiyo ambayo inakabiliwa upungufu mkubwa wa vitu muhimu.