Chuki:Viongozi waonywa Afrika Kusini

Haki miliki ya picha
Image caption waziri wa maswala ya ndani nchini Afrika kusini malusi Gigaba

Waziri wa masuala ya ndani nchini Afrika kusini ametoa wito kwa viongozi wa kitamaduni kukoma kutoa matamshi yasiyo na msingi ambayo yanaweza kusababisha maafa.

Waziri Malusi Gigaba amesema hayo baada ya mfalme wa Kizulu, Goodwill Zwelithini kusema kuwa wahamiaji wanapaswa kufunga virago vyao na kuondoka nchini humo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfalem wa Afrika kusini Goodwill Zwelithini

Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa zaidi ya wahamiaji elfu moja wameondoka kutoka mji wa mashariki mwa Durban katika kipindi cha siku chache zilizopita, kwa hofu ya kushambuliwa na raia wa nchi hiyo.

Raia wa kigeni hushambuliwa mara kwa mara nchini Afrika Kusini.