Pakistan kutounga upande wowote Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bunge la Pakistan

Bunge la Pakistan limeidhinisha mswada kuwa taifa hilo halitaegemea upande wowote katika mzozo unaokumba taifa la Yemen, licha ya ombi kutoka kwa utawala wa Saudia kuwa Pakistan ijiunge na muungano unaoendeleza mashambulio ya anga dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi.

Kwa mujibu wa azimio hilo, Pakistan haitaunga mkono upande wowote ili kuimarisha juhudi zake za kidiplomasia za kusaidia kumaliza mzozo huo licha ya ombi hilo kutoka kwa Saudi Arabia.

Lakini mkataba huo pia unasema kuwa iwapo ardhi ya Saudi Arabia itaingiliwa ,Islamabad itasimama bega kwa bega na taifa la Saudia na raia wake.

Waasi hao wa Houthi ambao ni wa madhehebu ya kishia wanaonekana kama kuungwa mkono na Iran ambayo imeagiza pakistan kukataa ombi hilo la Saudia.