Modeli aliyeishi kama mhamiaji haramu US

Image caption Mwanamitindo Iman Abdulmajid

Iman Abdulmajid aliishi nchini Marekani kama mhamiaji haramu.

Kulingana na mtandao wa yahoo,mrembo huyo kutoka nchini Somalia ambaye ameolewa na mwanamuziki David Bowie tangu mwaka 1992-aliingia nchini Marekani kwa kuidanganya serikali kuhusu umri wake kwa kuwa alikuwa mdogo mno kusafiri kutoka Kenya bila wazazi wake ambao hakuwa nao.

Iman:Nilidanganya na kusema kuwa nilikuwa na umri wa miaka 19 ili kupata pasipoti kwa kuwa bila hivyo ningelazimika kupata rukhsa kutoka kwa wazazi wangu na wazazi wangu hawangeniruhusu mimi kwenda Marekani.

Mbali na kuidanganya serikali hiyo mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 59 pia aliwadanganya wazazi wake kwa makusudi kuhusu kule aliko.

Iman alitarajiwa kuwa chuo kikuu cha Nairobi wakati alipoelekea New York ,kwa hivyo alidhani kwamba wazazi wake hawatagundua kule alikokwenda lakini baada ya mda mfupi baba yake alimuona katika gazeti la Newsweek.

Akizungumza na Gazeti la New York,Iman alisema:Ni Gazeti hilo analosoma baba yangu na alipokuwa akisoma aliona picha yangu na maandishi kwamba ''ndiye mwanamitindo mrembo kwa sasa''.

Nilivunja sheria lakini hakuna mtu ambaye anaweza kunishika hivi sasa, alijigamba mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60.