Nigeria kuchaguwa magavana na wabunge

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Raia wa Nigeria kupiga kura ili kuwachagua wabunge

Wapiga kura nchini Nigeria watapiga kura leo kuchagua magavana wa majimbo pamoja na wabunge.

Chama cha APC kinatarajiwa kupata ushindi mkubwa baaada ya mgombea wake wa urais Muhammadu Buhari kumshinda rais Goodluck Jonathan wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo chama cha bwana Jonathan cha PDP kinatarajiwa kupata ushindi kwenye maeneo mawili likiwemo eneo la Lagos ambalo huchangia theluthi moja ya uchumi wa Nigeria pamoja na jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers.

Usalama unatarajiwa kuwa wa juu kutokana na hofu ya mashambulizi kutoka kwa kundi la Boko Haram.