Saudia:Uamuzi wa Pakistan hautatuathiri

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mfalme wa Saudi Arabia katikati

Saudi Arabia imesema kuwa uamuzi wa Pakistan wa kutojiunga kwenye kampeni ya kijeshi inayoiongoza nchini Yemen hakutaiathiri kampeni hiyo.

Jeshi la Saudi Arabia linasema kuwa wanajeshi wa Pakistan wangesaidia tu likiongeza kuwa kampeni yake ya mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi inaendelea vyema.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Riyadh anasema kuwa mashambulizi hayo yameshindwa kuzuia waasi hao kusonga mbele na uamuzi wa Pakistan wa kutoegema upande wowote ni pigo kwa Saudi Arabia.