Hofu ya shambulizi yazua mauti Kenya

Haki miliki ya picha APTN
Image caption Baadhi wa chuo kikuu cha Garissa waliotoroka shambulizi la alshabaab

Mwanafunzi mmoja amefariki na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa baada ya kukanyagana katika chuo kimoja kikuu nchini Kenya.

Wanafunzi hao walibabaika baada ya kudhania mlipuko uliotokea katika mti wa stima ulikuwa wa shambulizi la kigaidi.

Walitoroka vyumba vyao vya kulala huku wengine wakiruka kutoka madirishani.

Siku kumi zilizopita watu 148 waliuawa katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa alshabaab katika chuo kimoja nchini Kenya.