Islamic State waharibu mji wa Nimrod

Haki miliki ya picha ap
Image caption Mwanamgambo wa Islamic State akiharibu sanamu

Wanamgambo wa Islamic State wametoa kanda ya video kupitia kwa mtandao ikiwaonyesha wakiharibu maeneo ya thamani kubwa kwenye mji wa Nimrod nchini Iraq.

Picha za wanamgambo hao wakitumia misumeno ya umeme kukata sanamu, zinaonekana kuthibitisha ripoti za mwezi uliopita kutoka kwa maafisa nchini Iraq kuwa wanamgambo hao wameharibu mji wa kitamadanu wa Nimrod.

Wanamgambo hao hutumia tinga tinga na milipuko kuharibu mji huo ambao wakati mmoja ulikuwa ni mji mkuu wa himaya ya Assyrian.