Somalia yapinga kuhamishwa kwa wakimbizi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kambi ya wakimbizi wa kisomali ya Dadaab

Serikali ya Somalia imesema kuwa kutakuwa na madhara makubwa iwapo Kenya itatekeleza uamuzi wake wa kuwahamisha mamia ya maelfu ya wakimbizi wa kisomalia nchini Somalia.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Somalia Abdisalam Omar amesema kuwa Kenya haijaiambia Somalia kuhusu mpango huo ambao ameutaja kuwa haramu.

Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto aliupatia miezi mitatu umoja wa mataifa kuwahamisha wakimbizi hao .

Tangazo hilo lilijiri siku chache baada ya shambulizi la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la alshabaab na kusababisha vifo vya watu 148 .somalia map