Maandamano ya kuwakumbuka mabinti wa Chibok
Huwezi kusikiliza tena

Nigeria yaadhimisha mwaka 1 wa Chibok

Ni mwaka mmoja sasa umetimia tangu wasichana zaidi ya mia mbili walipotekwa nyara na kundi la Boko Haram la nchini Nigeria. Wasichana hao walitekwa nyara tarehe na mwezi kama wa leo mwaka wa jana kutoka katika shule yao ya Chibokiliyoko katika jimbo la Borno.

Mpaka sasa haijajulikana hasa ni wapi walikofichwa wasichana hao.na tangu wakati huo kumekuwa na harakati zilizokuwa zikiendelea kushinikiza wasichana hapo waachiliwe kwa kauli mbiu ya #BringBackOurGirl kampeni ambayo imesambaa ulimwengu mzima na sasa ulimwengu unawakumbuka wasichana hao leo tunapoadhimisha mwaka mmoja tangu kutoweka kwao.

Na kampeni hizi lengo na nia yake ni kuukumbusha ulimwengu kuwa, wasichana hao zaidi ya mia mbili bado wako kizuizini kwa mwaka mmoja sasa.Kufuatia hali hiyo Mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na Mkaazi wa jiji la Lagos nchini Nigeria,Judith Mwikali kutaka kujua taarifa za kuonekana kwa mabinti hao upande wa kaskazini mwa nchi hiyo zina ukweli wowote?.