Wamiliki wa Hawala wahojiwa Kenya

Image caption Wamiliki wa Hawala zilizofungwa kwa kufanikisha Al Shabaab Kenya wahojiwa

Kufuatia shambulizi la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa, Serikali ya Kenya ilifunga akaunti za benki za watu na mashirika yapatayo tisini juma lililopita kutokana na madai kuwa huenda zinatumika kufadhili ugaidi.

Kwanzia leo hadi mwishoni mwa wiki, wanatakiwa kufika mbele ya Idara ya ujasusi kujieleza na kujitetea kuhusu tuhuma zinazowakumba za kufanikisha ugaidi

Kwanzia mwendo wa saa tatu asubuhi hii leo, wenye akaunti zilizofungwa wakiandamana na mawakili wao walianza kuwasili katika tawi

la idara ya ujasusi katika eneo la South C jijini Nairobi.

Image caption Serikali ya Kenya inadai Hawala zilizofungwa zilikuwa zinatumika kufadhili mipango ya Al Shabaab

Asilimia kubwa ya waliofika ni wenye asili ya kisomali.

Walielekezwa katika chumba cha faragha chini ya ulinzi mkali mmoja baada mwingine.

Albashir Hassan Aden ni mmoja aliyeathirika'' mimi nilikuwa wakala wa kuuza sukari na hakuna hata siku moja niliyojihusisha na kundi la Al Shabaab.

Kama ningekuwa na uhusiano nao ningejificha singekuwa hapa.

Nimekuja hapa ilinisafishe jina langu''alisema Hassan.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Al Shabaab ilikiri kuua wanafunzi takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa

Wengi wao walishtuka kuona majina yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wa Serikali.

Na walighadhabishwa na jinsi serikali ilivyowasilisha ujumbe huo.

Kutokuwepo kwa mawasiliano rasmi ya moja kwa moja iliwafanya wengi wao kuwa na wasiwasi kuhusu nia ya serikali ya kuandaa kikao hiki.

Kwa kawaida mtu akipatana na makosa nchini Kenya, huwa anatiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka kortini. Lakini wakati huu mambo yalikuwa tofauti kidogo. i.

''Serikali ilikosea mimi sio wakala wala chochote wa al Shabaab''.

''Afadhali ningeshauriwa na serikali kabla jina langu halijatajwa katika vyombo vya habari''.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Moja ya Hawala

''Kwa sasa hata hela za matumizi hazipo hata majukumu kama vile usafiri sina'' alisema mtuhumiwa mwengine Abdul.

Serikali ya Kenya ilitangaza hatua kadhaa za kiusalama mara tu baada ya shambulizi la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa .

Miongoni mwa hatua hizo zikiwa ni za kufunga akaunti za za watu binafsi na mashirika themanini na tisa.

Baadaye serikali iliwataka wale wote walioathirika na hatua hiyo kufika katika idara ya ujasusi kujieleza.