Iran yakomesha ibaada ya Umra Mecca

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran yakomesha Hija ya Umra Mecca na Medina

Huku uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia, ukiendelea kusambaratika, kuhusiana na mzozo wa kisiasa nchini Yemen,

Utawala wa Tehran, umetangaza kusitisha safari zote za hija kuelekea Mecca na Medina.

Kwa mujibu wa serikali ya Iran, raia wa nchi hiyo hawataruhusiwa kuelekea Saudia kwa maadhimisho ya Umrah,

kufuatia kudhulumiwa kwa wanaume wawili, raia wa nchi hiyo, wakati walipokuwa wakirejea nyumbani katika uwanja wa Jedda, mwezi uliopita.

Kashfa hiyo iliyohusiana na mzozo wa ngono na maswala ya kidini umepalia makaa katika mgongano wa kisiasa katika ya mataifa hayo mawili hasimu katika eneo la mashariki ya kati.

Mamia ya wairan waliandamana hadi nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran wakitaka serikali ya taifa hilo kushinikiza

Saudia kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo ya ngono.

Waziri wa turathi za taifa wa Iran Ali Jannati, amesema kuwa serikali ya Saudia imewatia mbarani watuhumiwa hao.

Takriban raia nusu milioni wa Iran huzuru Saudi Arabia kila mwaka kuadhimisha Umrah

Tehran na Saudia Arabia zinaunga mkono pande hasimu katika vita vinayoendelea huko Yemen na ilikuwa inatarajiwa kuwa raia wachache mno wa Iran watasafiri kuhiji mjini Mecca.