Hatimaye waliombaka Liz wahukumiwa Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hatimaye haki imetendeka baada ya watu watatu waliombaka msichana mdogo Liz kuhukumiwa kifungo cha mika 15 jela nchini Kenya

Mahakama moja mjini Busia, imewahukumu washukiwa watatu vifungo vya kati ya miaka saba na kumi na tano gerezani,baada ya kuwapata na hatia ya kumbaka na kumjeruhi msichana mmoja, aliyefahamika kama Liz.

Liz inasemekana alishambuliwa na vijana hao na kubakwa wakati alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa mazishi ya babu yake katika eneo la Busia Magharibi mwa Kenya.

Tukio hilo lilizua mjadala mkali nchini Kenya huku wanaharakati wa kijamii wakishinikiza serikai kuwachukulia washukiwa hao hatua kali.

Watatu hao walikuwa wamehukumiwa ''kufyeka nyasi katika kituo cha polisi'' na kuachiliwa huru.

Hata hivyo msichana huyo alikuwa amepooza kiwiliwili chake kuanzia kiunoni kufuatia kutupwa katika shimo ilikuficha ushahidi alipata

msaada baada ya wanaharakati wa kupigania haki za kibiniadamu kuishinikiza polisi kuchukua hatua dhidi ya polisi waliotoa hukumu hiyo nyepesi dhidi ya watu hao watatu.

Image caption Mamake Liz ameiambia BBC kuwa hatimaye haki imetendeka.

Mamake Liz ameiambia BBC kuwa hatimaye haki imetendeka.

Watatu hao sasa wamepatikana na hatia ya kumjeruhi Liz na kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 Jela.

They were also found guilty of causing bodily harm and sentenced to 7 years in prison.

Harakati za kumtafutia haki msichana huyo ziligonga vichwa vya habari mwaka uliopita watu zaidi ya miklioni 2

kote duniani walipotia sahihi kampeini ya kumlazimisha Inspekta mkuu wa Polisi

kuwachukulia hatua watatu hao ambao walikuwa wamedaiwa kuwahonga maafisa polisi huko Busia Magharibi mwa Kenya.