Sera ya EU kuzuia wahamiaji yakosolewa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji kutoka Afrika wakiwasili katika kisicha cha Lampedusa, Italia baada ya kuokolewa na walinzi wa pwani ya Italia Machi 24,2011

Nchi za Umoja wa Ulaya,EU, zimeshutumiwa kwa kuhatarisha maisha ya maelfu ya watu kutoka Afrika wanaotaka kuingia Ulaya kwa njia ya bahari.

EU imepunguza kwa kiasi kikubwa operesheni za uokoaji, ikisema inataka kuzuia wahamiaji wanaojaribu kuvuka bahari.

Lakini Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu wameonya kuwa sera hiyo imeshindwa.

Katika tukio la hivi karibuni watu wapatao mia nne wanaohofiwa kufa maji wakati boti yao ilipokuwa imepinduka katika bahari ya Mediterani. Walinzi wa pwani ya Libya, ambako wengi wa wahamiaji huanzia safari zao za hatari, wanasema wanatarajia mamia zaidi ya watu watasafiri katika siku zijazo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri.