Mauaji ya Imam:Msikiti wapekuliwa London

Image caption Mauaji ya imam mjini London, Polisi waupekua msikiti

Polisi mjini London wamekuwa wakiupekua msikiti ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wake wa mauaji ya Imam mmoja wa zamani kutoka Syria.

Abdul Hadi Arwani alipigwa risasi na kuuawa wiki moja iliopita katika makaazi ya Wembley mjini London.

Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa jamii ya waislamu ili kuwahakikishia kwamba upekuzi huo huo ni muhimu, na kwamba msikiti huo utafunguliwa haraka iwezekanavyo.

Abdul Arwani ameripotiwa kuwa mpinzani wa rais Assad wa Syria.

Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.