Mda wa kupiga kura waongezwa Sudan

Image caption Uchaguzi nchini Sudan

Tume ya uchaguzi nchini Sudan inasema kuwa imeongeza mda wa kupiga kura ya urais na ubunge hadi siku ya alhamisi huku ripoti za idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza zikitolewa.

Kura hiyo imesusiwa na upinzani ambao unasema kuwa idadi hiyo ya wapiga kura inaonyesha raia hawajali na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba rais Omar Al Bashir atatangazwa mshindi.

Bwana Al Bashir amekuwa mamlakani tangu mwaka 1989.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Sudan Omar Al Bashir

Shughuli ya upigaji kura ilitarajiwa kuchukua siku tatu na kukamilika leo.

Mkuu wa tume ya uchaguzi alisema kuwa alitarajia idadi ya wapiga kura ijitokeze na kufikia asilimia 45.