Wahamiaji wazidi kuokolewa Italia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmoja wa wahamiaji mama mjamzito akiokolewa pwani ya Italia

Walinzi wa pwani ya Italia wamesema kuwa karibu wahamiaji elfu kumi waliokolewa wiki iliyopita pekee wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterani kuelekea Ulaya, huku wahamiaji mia tisa wakiokolewa Alhamisi wiki hii.

Katika tukio lingine la kusikitisha, wahamiaji arobaini zaidi walikufa maji wakijaribu kufanya safari kutoka Afrika kwenda Ulaya.

Walionusurika wamesema boti yao ilizama.

Katika tukio lingine, polisi nchini Italia limekikamata kikundi cha wahamiaji wa Kiislam kutoka Ivory Coast, Mali na Senegal. Wanatuhumiwa kuwatuma majini Wakristo kutoka Nigeria na Ghana baada ya kuzuka ugomvi juu ya masuala ya dini.