Gesi ya chlorine yatumika Syria

Haki miliki ya picha SHAM NEWS NETWORK
Image caption Mtoto aliyeathirika na shambulizi la kemikali

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limetoa kanda yenye ushahidi inayoonyesha matumizi ya gesi ya chlorine kwenye shambulizi moja mwezi uliopita nchini Syria.

Kanda hiyo inaonyesha watoto watatu walio chini ya miaka minne ambao walikufa licha ya kuwepo jitihada za kuwakoa.

Daktari raia wa Syria ambaye aliwatibu watoto hao kwenye hospitali moja iliyo mkoa wa Idlib aliuambia mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kumekuwa na visa kadha vya mashambulizi ya gesi mwezi mmoja uliopita.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power anasema kuwa ni serikali tu ya rais Bashar al-Assad iliyo na helkopta zinazotumiwa kudondosha mapipa yenye milipuko iliyo na kemikali hatari.

Awali serikali ya Syria imekana madai hayo ikayataja kuwa propaganda.