UN:Yemen inahitaji msaada wa dharura

Image caption Umoja wa mataifa

Jumuiya ya Umoja wa mataifa imetoa ombi maalum kwa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa ajili ya kuisaidia Yemen, huku mapigano yakiongezeka na pia mashambulio ya angani katika sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Shirika la utoaji msaada la OCHA linapania kuchanga zaidi ya dola milioni mia mbili na sabini katika kipindi cha miezi mitatu ijao ili kushugulikia msaada huo wa dharura.

Shirika hilo linasema kuwa takriban watu elfu mia moja na hamsini wanaaminika kufurushwa makwao, asilimia hamsini zaidi ya hapo awali.

Mgogoro wa Yemen umekuwa m'baya zaidi tangu waasi wa Houthi walipomfurusha mamlakani Rais Abdrabuh Mansour Hadi mapema mwaka huu.