Washukiwa wa ugaidi wakamatwa Australia

Haki miliki ya picha police
Image caption Mshukiwa wa ugaidi nchini Australia

Polisi katika jimbo la Victoria nchini Australia wanasema kuwa wamewakamata wanaume watano kufuatia oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi kwenye mji wa Melbourne.

Wawili kati ya wanaume hao walio na umri wa miaka 18 walikamatwa baada ya kushukiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi yaikiwemo ya kuwalenga polisi.

Mshukiwa mwingine naye alikamatwa kufuatia sababu zinazohusiana na silaha. Shughuli za kuwatafuta washukiwa wengine zinaendelea sehemu zingine za mji wa Melbourne.