Mwili wa Al Douri kufanyiwa uchunguzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Izzat Ibrahim A Douri

Uchunguzi wa chembechembe za DNA unatarajiwa kufanyiwa kile maafisa nchini Iraq wanasema kuwa ni mwili wa Izzat Ibrahim al Douri ambaye ni mwanachama wa mwisho wa uliokuwa utawala wa Saddam Hussein ambaye amekuwa akitafutwa.

Maafisa wa jeshi wanasema kuwa aliuawa na vikosi vya serikali wakati msafara wake uliposhambuliwa karibu na mji wa Tikrit

Bwana al Douri anaaminika kuchangia pakubwa katika ukuaji wa kundi la Islamic State nchini Iraq.

Aliyekuwa msemaji wa chama cha Baath ambacho kilikuwa chama chake al - Douri alikana kuuawa kwake.